Mnamo septemba 24 tulitembelea SHULE YA SEKONDARI HALISI iliyoko Gongo la mboto eneo la Majohe. Lengo kuu ya ziara ilikuwa kusoma kwa kushirikiana na wanafunzi wa shule wa Sekondari Halisi wa kidato cha tatu na nne.

Tulianza kujifunza somo la Kiswahili ikifuatiwa na Lugha ya Kiingereza, Uraia na Biolojia. Tulianza Kiswahili ambalo ni lugha ya taifa.

Mwalimu wa Kiswahili wa shule wa Halisi aliitwa Madam Halima na mwalimu wa shule wa AMSB aliitwa Mwalimu Othuman Yahya. Katika kipindi hii tulisoma mada wa Uhakiki wa kazi ya fasihi kwa kujadili Tamthilya ya Kilio Chetu na Orodha.

Somo lililofuata ni la Uraia(Civics). Mwalimu wa Civics wa shule wa Halisi aliitwa Madam Mwamini Bakari na mwalimu wa shule wa MSB aliitwa Mwalimu Malick Mpita. Katika civics tulisoma mada wa uchaguzi wa kidemokrasia na mwaka huu uchaguzi utafanyika tarehe ishirini na nane mwezi wa Octoba.

Pia tulisoma Lugha ya Kiingereza. Mwalimu wa Kiingereza wa shule wa Halisi waliitwa Madam Mlay na Madam Pendo na mwalimu wa shule wa AMSB aliitwa Mwalimu Madam Fatema Hassan. Katika kipindi hii tulisoma mada wa Uhakiki wa kazi ya fasihi kwa kujadili Riwaya ya Unanswered Cries.

Kutoka hapa tulipata mapumziko ya dakika ishirini. Wengi (sisi na wanafunzi wengine wa Halisi) tulielekea kantini kwajili kupata chai kwa kushirikia na wanafunzi wenzetu.

Baada ya mapumziko tulikuwa na kipindi cha Biologia cha kwenda Maabara. Mwalimu wa Halisi aliitwa Mr. Hassan na Mwalimu wa AMSB aliitwa Mr. Talanta. Hapa tulisoma mada wa Uratibu(Coordination). Tulipewa Karatasi za maelekezo na maswali ikisema kuangalia Ulimi wetu na kutambua sehemu za ladha tofauti.
Kipindi chote kilikuwa cha dakika arobaini na tano na kiliishia vizuri kama ilivyopangwa.

Tulipomaliza masomo tulikwenda kucheza michezo mbalimbali, hususan mpira wa mguu na mpira wa kurushiana. Mpira wa miguu ulichezwa na wanaume tu, na

mpira wa kurushiana ilichezwana na wasichana. Hii michezo imenifurahisha sana kubadilisha mawazo ya shule hii kwa sababu tanapata elimu ya michezo na masomo vilevile.

Kusudi la ziara hii ilikuwa ya kusoma na kuzalisha/ kubadilishana uzoefu na mazoezi mazuri kati ya shule unayotembelea na shule unayotoka. Kwa hivyo Kushiriki katika ziara ya kujifunza, inaweza kuzidisha uzoefu wa kufurahisha na ala muhimu ya kujifunza kwako.

 Tunafurahi sana kuwa tulipata nafasi ya kusoma kama mwanafunzi katika shule halisi ya sekondari kwa siku moja. Tulikuwa na muda mzuri kutembelea shule hiyo kwa sababu tulipata uzoefu wa kusoma kutoka kwa waalimu tofauti. Kujifunza uzoefu anuwai wa maisha katika nyanja kadhaa..

Zaidi ya hayo ziara hii tulipata nafasi ya kushirikiana na wanafunzi wa sekondari ya halisi na kuunda urafiki kati yao. Ninaamini kuwa ili mtu ajifunze vyema lazima atategemea kupata mazingira mazuri, hivyo katika ziara yetu ya shule hiyo tuliona mazingira ambayo wanafunzi walikuwa wakisoma, yalikiwa safi.

Ninahitmisha kusema kwamba tumebadilishana mawazo kwenye masomo na michezo ili elimu yetu iwe na mwanufaa. Ujifunzaji ni mchanganyiko wa mazingira yanayosaidia, walimu waliojitolea na wanafunzi ambao wanafurahi katika kujifunza. Kwa hivyo kwa ziara hii, tulipata fursa ya kukutana na wanafunzi tofauti wa shule tofauti. Ningependa tubadilishane mawazo kila mara. Ni hasa ya elimu yetu, inafanya iwe rahisi kwako kujua wenzako wanapata elimu gani na hali yao ya mazingira ya shule. Tunashukuru juhudi za waalimu wetu katika kuandaa safari ya kushangaza ambaye ilituwezesha kushiriki uzoefu kadhaa na mwanafunzi mwenzetu wa SHULE YA SEKONDARI YA HALISI.

ASANTE
Ripoti imeandikwa na:
Mwalimu. OTHOMAN YAHYA,
Mwanafunzi. SAKINA HATIM KADERBHAI,
Mwanafunzi. HATIM JUZER KADERBHAI.

Back to top