Magufuli we mpendwa,
Sisi tunakukumbuka,
Duniani kutuaga,
Kwa mungu nakuombea.

 

Watanzania twalia,
Ua letu kunyauka,
Gizani kutuachaga,
Nenda Baba Tangulia.

 

Kwako tumejifunzaga,
Upendo kutuonyesha,
Umoja tuleteaga,
Hatukusahau baba.

 

Miundombinu kujenga,
Reli pia barabara,
Ndege kuzinunuaga,
Tunakushukuru kwa yote.

 

Ulionyesha msimamo,
Kutetea wasonacho,
Maskini kua nao,
Nenda baba tangulia.

 

Raisi wangu Samia,
Rekodi umeifunja,
Wanawake kupaisha,
Taifa kulikamata.

 

Wewe ni mtu makini,
Hata mungu ni shahidi,
Usiogope majini,
Hawatakuweza kamwe.

 

Shule umeshaisoma,
Na elimu umeipata,
Sisi hatunaga shaka,
Gari utaiendesha.

 

Wakamate wala rushwa,
Matumbo kuyashibisha,
Tengeneza na viwanda,
Nakuombea kwa mungu.

 

Elimu bure kutoa,
Miradi kuendeleza,
Reli umeme fatiha,
Ziba mianya ya wezi.

 

Hospitali kuzijenga,
Maji na kuwa patiya,
Ufisadi kupambana,
Hapo nchi utaiweza.

 

Tamati ninaishia,
Majonzi yananipata,
Yote namwachia mungu,
Kwaheri baba Magufuli hatutakusahau.

 

Written by Abbas Gohar

Form 4

Back to top