Umetuongoza vizuri
Wewe shujaa
Ushatuacha
Macho yamejaa

 

Ulikuwa na msimamo
Wenye ajabu
Uzalendo wako
Ni kama dhahabu

 

Siku yoyote
Hujatishwa
Waliojaribu kukutisha
Wale wamekwisha

 

Tanzania iende mbele
Ilikuwa milengo yako
Umejenga imara
Shukrani kwako

 

Sisi hatujaamini
Saa tulisikia
Ulituacha wewe
Moyoni utabakia

 

Wale wajakupenda
Ubaya kwao
Sisi tulikuwa pamoja
Magufuli babalao

 

Kila kitu ulitufanyia
Ile hayasahauliki
Ukae na amani
Mungu akubariku

 

Ushaondoka
Daima tutakumbuka
Salamu kwako
Shujaa wa Afrika

 

written by Murtaza Zavery

Form 4

 

Back to top