wanafunzi wa kidato cha tatu na cha nne wa shule ya sekondari ya AL- MADRASA TAREHE 24/9/2020 tulifanya ziara ya kielimu kwenda katika shule ya sekondari ya HALISI iliyopo katika wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar-es-saalam katika eneo la MAJOHE. Tuliondoka mnamo saa TATU na kufika saa nne na robo.

KUINGIA DARASANI
Kwa vile lengo kuu la ziara hiyo ni kujifunza taaluma ya masomo, hivyo tuliingia darasani na kufundishwa masomo ya KISWAHILI,(Tulifundishwa na Mwl. Halima Mrisho na A.Yahya) CIVICS (Tulifundishwa na Mwl. Mwamini Bakari na Malick Mpita) na ENGLISH(Tulifundishwa na Mwl. Mlayi na Pendo) walimu wote wa shule zote mbili walishirikiana katika kutufundisha. Wanafunzi wote kwa ujumla tukiwa darasani tulifurahia sana kwani tuliweza kupata maarifa na ujuzi wa masomo haya.

MASOMO KWA VITENDO
Baada ya mapumziko ya muda mfupi wanafunzi tulikwenda kwenye maabara ya somo la BAIOLOJIA ambapo tuliweza kufundishwa somo hilo kwa vitendo na mwalimu Said.

MCHEZO WA MPIRA
Baada ya masomo wanafunzi wote tulikwenda kiwanjani kwa lengo la kucheza mpira wa miguu na wa pete, katika michezo hiyo kulikuwa na ushindani mkubwa sana na matokeo yake ni kuwa, katika mpira wa miguu shule ya AL- MADRASA SEKONDARI ilishinda kwa goli moja kwa bila dhidi ya HALISI sekondari, na kwa upande wa mpira wa pete timu zote zilitoka sare.

Ahsante
Mwalimu wa Kiswahili

Back to top